Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wa vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo hazikuwa na vyuo hivyo, pamoja na chuo kimoja kinachojengwa Kigamboni. Jumla ya vyuo vinavyojengwa ni 65.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema hayo Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro katika ziara ya Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba kukagua ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani humo.
Amesema tamko la ujenzi wa vyuo hivyo lilitolewa Juni 14, 2022 wakati wa bajeti kuu ya Serikali, ambapo Sh100 bilioni zilitengwa kwa ajili ya kuanza mradi huo katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Mpango huo unatokana na maelekezo ya Rais ambaye alitaka kila wilaya isiyokuwa na chuo cha VETA ipate, pamoja na kila mkoa usiokuwa na chuo cha mkoa kujengewa.
(Feed generated with FetchRSS)