#VIDEO: Azam FC imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuifunga Yanga SC mabao 3-2 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za kawaida kabla ya Azam FC kupata bao la ushindi katika muda wa nyongeza na kufuzu hatua inayofuata.
Baada ya mechi hiyo, viongozi wa timu zote mbili walizungumza kuhusu matokeo na mwenendo wa mchezo, huku kila upande ukieleza mtazamo wake kuhusu pambano hilo na malengo ya timu zao kuelekea mechi zilizosalia msimu huu.
Kwa ushindi huo, Azam FC sasa itaungana na Simba SC katika mchezo wa fainali ya CRDB Federation Cup msimu wa 2025/2026, pambano ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kati ya vigogo hao wa soka la Tanzania.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania
Capitalradio Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)