#HABARI: Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda, amewataka wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) nchini kuanza kutoa huduma kwa saa 24 ili kuendana na kasi ya Forodha na kurahisisha biashara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Februari 19, 2026, Kamishna Mwenda amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano wa mizigo na kuongeza ufanisi, huku akiahidi kuwa TRA itatoa watumishi wa kutosha kuwezesha utaratibu huo kuanza mara moja.
Pamoja na kutoa agizo hilo, Kamishna Mkuu ameonya vikali dhidi ya vitendo vya ukwepaji kodi vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa ICDs, akisisitiza kuwa TRA ina taarifa za kutosha na haitasita kuchukua hatua za kisheria.
Amesema ufanisi wa bandari hizo ni muhimu kwani Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Juma Bakari, amebainisha kuwa asilimia 52 ya mapato ya forodha yanatokana na Bandari Kavu, jambo linalohitaji ushirikiano wa karibu na uzingatiaji wa sheria.
Kwa upande wao, wadau wa sekta binafsi kupitia Rais wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula, wamesisitiza kuwa ICDs ni kiungo muhimu kuelekea Dira ya Taifa ya 2050, huku Mwenyekiti wa Wamiliki wa Bandari Kavu, Bw. Meleckzedeki Kichange, akipongeza matumizi ya mifumo ya kidigitali kama TANCIS.
Kichange ameeleza kuwa kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira bora ya amani na utulivu kuliko kipindi kingine chochote, na wapo tayari kuendelea kushirikiana na TRA kuleta mapinduzi ya kiuchumi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania