#HABARI: Mvua iliyonyesha kwa muda mfupi katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam imesababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara ya Mandela, hususan katika eneo la Sokota.
Maji mengi yametuama barabarani na kupelekea magari na watembea kwa miguu kupita kwa shida, hali iliyoibua changamoto kubwa ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kutokana na kujaa kwa maji hayo, foleni ndefu imejitokeza katika barabara hiyo muhimu inayounganisha maeneo mbalimbali ya jiji.
Watumiaji wa barabara wamejikuta wakitumia muda mrefu njiani, jambo linaloashiria hitaji la kuboreshwa kwa mifumo ya mifereji ya maji ili kuzuia adha kama hizo nyakati za mvua.
Barabara nyingine iliyo athiriwa na mvua hiyo ni ile ya United Nation katika eneo la Upanga barabara inayotumika kuelekea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.