Vijana wa Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na kongamano lililoandaliwa na programu ya Tanga yetu kwa Kakupitia, Halmashauri ya Jiji la Tanga lenye lengo la kuwawezesha kujitambua, kujiamini na kutumia ipasavyo fursa za maendeleo kwa ustawi wao na jamii kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa Kongamano la Vijana linalofanyika katika Viwanja vya Lamore, jijini Tanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji ya Tanga Yetu, Rashid Iddi, amesema kongamano hilo limeandaliwa kwa lengo la kuwajengea vijana uwezo wa kujitambua, kuhamasika kutumia fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii na uchumi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Masuala ya Afya ya Akili katika Mtandao wa Vijana Togora, Sadaka Saidi, amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo, akisema ni fursa muhimu ya kukutana na wataalamu kutoka sekta mbalimbali watakaowapa elimu, maarifa na mbinu za kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.

Baadhi ya vijana walioshiriki katika kongamano hilo wameeleza matarajio yao ya kunufaika na elimu mbalimbali zinazotolewa, ikiwemo mbinu za kujikwamua kiuchumi, ujasiriamali, matumizi ya fursa za maendeleo na stadi za maisha zitakazowasaidia kujenga mustakabali bora.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *