#HABARI: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wananchi katika utoaji wa fursa zinazotokana na miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kuhakikisha jamii inanufaika moja kwa moja na uwekezaji huo.
Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la taaluma katika kampasi ya Tanga ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Waziri Kikwete ameitaka jamii kuwekeza zaidi katika elimu, akisisitiza kuwa elimu ndiyo nguzo kuu ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa chuo hicho, Ernest Mabonesho, amesema lengo la taasisi hiyo ni kuwahudumia wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwajengea uwezo watumishi na wadau wa sekta ya umma ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Serikali imetenga shilingi Bilioni 39 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho, ambacho kitakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi elfu mbili, Kampasi hiyo inajengwa katika Mtaa wa Kasera, Kata ya Maweni, Jijini Tanga, na inatarajiwa kuongeza fursa za elimu pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa eneo hilo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania