#HABARI: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kennan Kihongosi, amewataka watumishi wa umma wilayani Kasulu kufanya kazi kwa uaminifu, upendo, na ushirikiano huku wakiepuka unafiki na migogoro mahali pa kazi.
Akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Kigoma, Kihongosi amesisitiza kuwa watumishi hawapaswi kutumia nafasi zao kukandamiza wengine au kuwanyanyasa wananchi, bali watumie dhamana hizo kuwatumikia kwa haki.
Wito huo umetolewa wakati kiongozi huyo akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, ambapo pia alitumia fursa hiyo kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Amewataka watendaji hao kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa viwango bora ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa kwa jamii na kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.