#HABARI: Serikali imezitaka taasisi za uhifadhi wa misitu na maliasili kuwekeza katika elimu tiba na kuanzisha kliniki maalum zitakazotumia asali, nyuki, na mazao yake kwa ajili ya matibabu ya wananchi na utalii.
Wito huo umetolewa mjini Morogoro na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande, alipozungumza na viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), ambapo alisisitiza kuwa matumizi ya chavua na sumu ya nyuki yana thamani kubwa katika tiba na viwanda vya dawa duniani.
Naibu Waziri Chande amewaagiza viongozi wa TFS kuongeza uzalishaji na usafirishaji wa asali ili kufikia malengo makubwa ya kibiashara na kuongeza mapato ya fedha za kigeni.
Alibainisha kuwa uwekezaji katika tafiti za kisayansi na ubunifu utasaidia kufikisha bidhaa hizo kwenye masoko ya kimataifa, jambo litakaloinua uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wafugaji nyuki nchini.
Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo, ameeleza kuwa taasisi hiyo imepata mafanikio makubwa katika mapato ya utalii ikolojia, ulinzi wa misitu, na matumizi ya teknolojia ya kisasa.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bernard Marceline, ameupongeza utendaji wa TFS na kuutaja kuwa wa mfano katika kuimarisha sekta ya misitu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.