#HABARI: Jumla ya vitongoji 474 kati ya 1,636 ambavyo havina umeme mkoani Kagera vinatarajiwa kuanza kunufaika na nishati ya REA ifikapo Februari 2029, kufuatia kuwasili kwa mkandarasi wa mradi huo.
Mhandisi Ernest Makale, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA, amemtambulisha mkandarasi huyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kuwafikishia wananchi huduma muhimu ya nishati vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Yahya Ramadhani Kido, amemtaka mkandarasi huyo kutekeleza mradi kwa wakati na kuhakikisha anasuluhisha migogoro yoyote itakayojitokeza ili kutoathiri kasi ya ujenzi.
Wananchi wa mkoa huo wameonyesha matumaini makubwa, wakieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika vitongoji vyao vilivyokuwa vimesubiri huduma hiyo kwa muda mrefu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.