#HABARI: Mkurugenzi Mkuu wa World Health Organization (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, anatarajiwa kuzindua jengo la kisasa la huduma kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) katika Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, jengo hilo limejengwa na Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Akizungumza kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Doris Mollel, amesema ujenzi wa jengo hilo umegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 2 na unalenga kuboresha huduma za kibingwa pamoja na miundombinu kwa watoto njiti, hususani katika Mkoa wa Mwanza, ambao una kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Amesema ushirikiano wake na Dk.Tedros ulianza mwaka 2024 ukiwa na lengo la kuitangaza ajenda ya watoto njiti katika jukwaa la Kimataifa na kuhamasisha uwekezaji zaidi katika huduma za afya ya mama na mtoto.

Kwa mujibu wa Doris, taasisi hiyo imejipanga kujenga hospitali 10 za kisasa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Shinyanga, Geita, Tabora na Zanzibar ifikapo mwaka 2028, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuboresha huduma za afya nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *