Chanzo cha picha, Getty Images
Wanafunzi katika vyuo vikuu kadhaa nchini Iran wamefanya maandamano ya kupinga serikali, maandamano ya kwanza ya aina hii kwa kiwango hiki tangu msako mbaya wa mwezi uliopita uliofanywa na mamlaka.
BBC imethibitisha picha za waandamanaji wakiandamana kwenye chuo kikuu cha Sharif katika mji mkuu Tehran siku ya Jumamosi.
Mapigano yalionekana baadaye yakitokea kati yao na wafuasi wa serikali.
Maandamano yalifanyika katika chuo kikuu kingine cha Tehran, na mengine yaliripotiwa kaskazini-mashariki.
Wanafunzi walikuwa wakiwaenzi maelfu ya wale waliouawa katika maandamano makubwa mwezi Januari.
Marekani imekuwa ikijenga uwepo wake wa kijeshi karibu na Iran, na Rais Donald Trump amesema anafikiria kufanya shambulizi dogo la kijeshi.
Marekani na washirika wake wa Ulaya wanashuku kwamba Iran inaelekea kuendeleza silaha ya nyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa ikilikanusha kila mara.
Maafisa wa Marekani na Iran walikutana Uswisi siku ya Jumanne na walisema kuwa maendeleo yalikuwa yamepatikana katika mazungumzo yaliyolenga kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.
Lakini licha ya maendeleo yaliyoripotiwa, Donald Trump alisema baadaye kwamba dunia itajua “katika siku 10 zijazo, huenda” kama makubaliano yatafikiwa na Iran au Marekani itachukua hatua za kijeshi.
Unaweza kusoma;