Mhadhiri wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Jackson Coy, amesema jamii inapaswa kufikiri zaidi ya mtazamo wa kawaida ili kuona thamani na mahitaji ya makundi yenye uhitaji maalum.
Amesema kufikiri kwa kina husaidia hata makundi yasiyo na uwezo wa kujisimamia au kujenga hoja zao, kama watoto na vijana wanaohitaji msaada, kupata kipaumbele na kujiona sehemu ya jamii.
Dkt. Coy ametoa wito huo leo, Februari 22, ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Kufikiri Duniani – World Thinking Day, inayolenga kuikumbusha jamii kuwajali na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ili nao wapate haki na fursa stahiki.
✍Ibrahimu Kilumbo
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)