Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu masuala ya kimataifa amesema: “Uchunguzi kuhusu kesi ya wanasiasa wa Marekani na washirika wao wa Magharibi katika kadhia ya Jeffrey Epstein umeibua kashfa kubwa katika nchi za Magharibi katika nyanja zote.”

Ali Akbar Velayati ameandika katika sehemu ya makala yake kuhusu kudhoofiika na kuporomoka ustaarabu wa Magharibi sambamba na kuibuka tena ustaarabu wa Kiislamu-Kiirani, kamba kashfa ya Epstein ni mwisho wa ustaarabu wa kimaonyesho wa Magharibi.

Ameongeza kuwa: “uchunguzi wa historia ya karne kadhaa zilizopita unaonyesha wazi kwamba ustaarabu wa Magharibi, bila kujali madai yake yasiyo na msingi eti ya kutetea haki za binadamu na maadili, umekuwa ukitegemea vurugu, unyonyaji na kuchochea vita.”

Amesema: Kuanzia kugawana dunia baina ya nchi za wakoloni kulikosimamiwa na Papa, hadi Vita vya Dunia vilivyosababisha vifo vya mamilioni ya watu, mauaji ya kimbari ya Bosnia kwa msaada wa Wazungu hadi mauaji ya watu wasio na hatia huko Gaza, yote yameunda msururu wa uhalifu unaoendelea leo hadi vita nchini Ukraine.

Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduizii ya Kiislamu katika Masuala ya Kimataifa ameashiria mfano wa Iran akilinganisha staarabu mbili za Mashariki na Magharibi na kusema: “Ustaarabu wa Kiislamu-Kiirani, pamoja na historia yake ya kale ya kupigania amani na haki, umebeba silaha tu kwa ajili ya kujilinda tangu wakati wa Cyrus, mwanzilishi wa nasaba ya Achaemenid, na siku zote umekuwa mtetezi wa kuishi kwa amani mataifa yote.”

Ali Akbar Velayati amesema: “Mchakato wa kujenga upya na kufufua ustaarabu wa Kiislamu ulianza kwa ujio wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran. Leo, ambapo kashfa za kimaadili na kisiasa za dunia ya Magharibi, kuanzia kesi ya Epstein hadi uungaji mkono wa wazi kwa mauaji ya kimbari huko Gaza, zimeamsha maoni ya umma ya duniani, wakati umefika wa kufafanua upya nafasi halisi ya ustaarabu, na kwa ulimwengu kujua kwamba mustakabali ni wa ustaarabu unaotambua haki, amani na utu wa binadamu, si kwa kauli mbiu bali kwa vitendo.” 

Kesi ya Jeffrey Epstein, mlanguzi wa ngono na bilionea aliyehusishwa na mtandao wa wanasiasa, wanadiplomasia na matajiri, imezusha tetemeko la kisiasa katika nchi za Magharibi. 

Wataalamu wanasema, “Mafaili ya Epstein” yana ushahidi wa kushtua na unaoaminika wa udhalilishaji wa kingono, biashara haramu ya binadamu na unyonyaji wa wanawake na wasichana kwa mtindo wa kimfumo na wa kimataifa.

Vitendo vilivyobainishwa kwenye mafaili hayo vinaweza kujumuisha utumwa wa kingono, ukatili wa uzazi, kutoweka kwa lazima, mateso, vitendo vya kinyama na vya kudhalilisha utu, pamoja na mauaji ya wanawake.

Wataalamu hao wamebainisha kuwa, uhalifu huo ulitendeka katika mazingira yaliyojaa ubaguzi wa rangi, rushwa, chuki kali dhidi ya wanawake, na mtazamo wa kuwafanya wanawake na wasichana kuwa bidhaa pamoja na kuwavua utu wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *