
Kamati ya vikwazo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imewaongeza maafisa wanne Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye orodha yake ya vikwazo kwa Sudan. Imelaani kuhusika kwao katika uhalifu na ukatili dhidi ya raia wa Sudan, hasa Darfur na El-Fasher. Mbinu hii ya shinikizo inahusisha tu kuzuia mali zao na kuwawekea vikwazo vya usafiri.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililozingatia mfululizo wa uhalifu ulioandikwa, ambao ulifanywa huko El-Fasher na kwa hivyo limeidhinisha kuongezwa kwa maafisa hawa wa ngazi za juu, akiwemo Abderrahim Dagalo, naibu mkuu wa RSF na kaka wa Mohamad Hamdane Dagalo, anayejulikana kama Hemedti. Ingawa anamiliki kampuni kadhaa nje ya nchi zilizosajiliwa katika Falme za Kiarabu, kuna uwezekano mkubwa kwamba mhusika hana wasiwasi wowote, kutokana na nafasi ya Abu Dhabi katika mzozo wa Sudan.
Gedo Hamdane Ahmed Mohamed, anayejulikana zaidi kama Abu Shuk, kamanda wa sekta ya Kaskazini mwa Darfur ya Vikosi vya Msaa wa Haraka, pia yuko kwenye orodha hii. Vile vile Tijani Ibrahim Moussa Mohamed, kamanda wa wa RSF, anayejulikana kama al Zeir Salem.
Maafisa watatu wa RSF wanakabiliwa navikwazo vya Uingereza, Marekani, na Ulaya
Hatimaye, Brigedia Jenerali Elfateh Abdullah Idris Adam, anayejulikana zaidi kama Abu Lulu, pia amechukuliwa vikwazo. Anajulikana kwa kupiga picha mauaji aliyoyafanya, hasa huko El-Fasher. Kufuatia malalamiko na shutuma baada ya kutekwa kwa mji huo, RSF ilidai kumkamata mwezi Oktoba mwaka uliyopita, lakini hatimaye alijitokeza tena siku mbili baadaye.
Siku ya Jumapili, Februari 22, alionekana katika video mpya huko Mostariha, mji ulioko Kaskazini mwa Darfur ukishambuliwa na RSF ambapo raia 28 waliuawa na wengine 40 kujeruhiwa, huku mamia wakitoroka makazi yao.
Maafisa watatu wa hivi karibuni wa RSF walioongezwa kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa tayari wanakabiliwa na vikwazo kama hivyo kutoka Uingereza, Marekani, na Umoja wa Ulaya (EU) kwa majukumu yao katika uhalifu na mauaji yaliofanywa Darfur. Watu hawa wapya wanne wanajiunga na viongozi wengine wawili wa RSF: Ali Othman Mohamad Hamed, mkuu wa operesheni, na Abderrahmane Jomaa Barkal, kamanda wa RSF huko Darfur Magharibi.