
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran yamepangwa kuanza tena siku ya Alhamisi, Februari 26, mjini Geneva. Pande zote mbili zinasema zinatoa kipaumbele njia za kidiplomasia, lakini uwezekano wa shambulio la Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hauwezi kuondolewa. Nchini Israel, kiwango cha tahadhari hakijabadilika kwa siku kadhaa. Hata hivyo, kupelekwa kwa jeshi la Marekani kunaangaliwa kwa karibu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Jerusalemu, Frédérique Misslin
Kufanya nguvu ionekane ili kutoa ushawishi katika mazungumzo: ndege kumi na mbili za kivita za Marekani za F-22 Raptor zilitua nchini Israel Jumanne, Februari 24. Kupelekwa kimkakati kwa ndege za kivita za Marekani na meli za kivita katika eneo hilo kunaonyesha kwamba Marekani na Israel zinajiandaa kwa tukio lolote. Huu ni uchambuzi wa Raz Zimmt, mtaalamu wa Iran katika Taasisi ya Masomo ya Usalama wa Kitaifa huko Tel Aviv:
“Ni wazi hili linalenga kuihimiza Iran kufanya makubaliano. Lakini lengo kuu ni kumpa Rais Trump uhuru wa kutosha kufanya uamuzi wowote anaotaka, iwe ni shambulio dogo au shambulio kubwa zaidi.”
Malengo ya vita ya Donald Trump bado hayajajulikana
Uwezekano wa makubaliano bado uko mezani, lakini Israel inaogopa suluhu ya haraka ambayo, kwa mtazamo wake, haitakuwa kamili: makubaliano ambayo hayatamaliza mpango wa nyuklia na yataacha uwezo wa makombora ya balestiki wa Iran ukiwa umebaki. Wachambuzi wanabainisha hatari ya kuongezeka kwa mgogoro wa kikanda haiwezi kuepukika.