Wapiga kura 127,632 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa kuchagua mbunge katika Jimbo la Peramiho Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa, Jacobs Mwambegele amesema jumla ya vituo 373 vya kupigia kura vitatumika ambako vyama vya siasa 15 vimesimamisha wagombea.
Jaji Mwambegele amesema vituo vitafunguliwa saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni. “Baada ya kumaliza kupiga kura, mpiga kura anatakiwa kuondoka eneo la kituo cha kupigia kura ambako wapiga kura wataruhusiwa kutumia moja ya vitambulisho; cha Taifa NIDA, Leseni ya udereva au Pasi ya kusafiria.
Wananchi wa Jimbo la Peramiho wanaenda kupiga kura kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jenista Mhagama kufariki dunia
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)