Chanzo cha picha, NurPhoto via Getty Images
“Hoja kuu ni wazi kabisa, Iran hairuhusiwi kumiliki
silaha za nyuklia. Ikiwa itachukua hatua za kutengeneza upya silaha hizo, hali
hiyo itakuwa changamoto kubwa kwetu. Kwa hakika, tumeshuhudia viashiria
vinavyoonesha kuwa wanaelekea katika mkondo huo,” amesema JD Vance, Makamu wa
Rais wa Marekani, kabla ya kuanza kwa duru mpya ya mazungumzo mjini
Geneva.
Makamu huyo wa Rais aliongeza: “Ndiyo sababu Rais ametuma
wajumbe wa majadiliano ili kushughulikia suala hili. Kama alivyorudia mara
kadhaa, anapendelea suluhu ipatikane kwa njia ya diplomasia; hata hivyo, bado
kuna mbinu nyingine zinazoweza kuzingatiwa endapo itahitajika.”
Katika saa zijazo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas
Araqchi, anayeliongoza ujumbe wa kidiplomasia wa nchi yake, anatarajiwa kufanya
mazungumzo na Steve Whittaker, mwakilishi maalum wa Donald Trump kwa Mashariki
ya Kati, jijini Geneva, Uswisi, kwa upatanishi wa Oman.
Soma Zaidi: