#HABARI: Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Mkoa wilayani Nkasi mkoani Rukwa, ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 90 na kwamba shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 320 kwa mwaka.
Mkuu wa wilaya hiyo Peter Lijualikali, amefanya ziara ya ukaguzi wa shule hiyo na kubainisha kuwa shule hiyo ina jumla ya majengo 13 ikiwemo mabweni, karakana na vyumba 8 vya madarasa na hadi sasa wanafunzi 51 wameripoti na kuendelea na masomo.
Aidha, amesema uwepo wa shule hiyo utawazesha wanafunzi kupata ujuzi kwa vitendo utakaowawezesha kupata ajira kwa haraka, kujiajiri, na kuongeza kipato ikiwa ni pamoja na kujitegemea kiuchumi na kupunguza ukosefu wa ajira.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.