#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Iringa, limekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Ibrahimu Myovella, na wenzake watatu wamepotea wakiwa mikononi mwa polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, SACP Allan Bukumbi, amefafanua kuwa watuhumiwa hao wanaokabiliwa na tuhuma za mauaji walikimbia polisi na hawashikiliwi kama inavyodaiwa, akiahidi kuendelea kutoa taarifa rasmi ili kuondoa sintofahamu miongoni mwa wananchi.
Awali, Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) lilieleza kusikitishwa na ukimya wa jeshi hilo, likidai kuwa viongozi wao walitoweka tangu waliporipoti Kituo cha Polisi Iringa Mjini Februari 18, 2026.
BAVICHA imelishutumu jeshi hilo kwa kuwashikilia viongozi hao kwa siku nane bila kuwafikisha mahakamani wala kuwapa dhamana, hali iliyozua hofu kubwa kwa familia zao na wanachama wa chama hicho.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.