
Kiongozi wa mtandao unaodaiwa kuwatuma Wakenya zaidi ya 1,000 kwenda Urusi, ambapo wengi waliandikishwa kwa nguvu jeshini, ameshtakiwa mnamo Februari 26, 2026, kwa “biashara ya binadamu,” ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Kenya imetangaza siku ya Alhamisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nchini Kenya, Festus Arasa Omwamba alikamatwa kwa “biashara ya binadamu.” Alishtakiwa siku ya Alhamisi na mahakama ya kupambana na ugaidi katika mji mkuu, Nairobi, kwa kuwasafirisha Wakenya 25 kwenda Urusi mwaka jana.
Jina lake liko katikati ya uchunguzi mpana kuhusu kuajiri raia waliotumwa kupigana katika safu ya jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Alifanya kazi kutoka Nairobi kupitia shirika lililosajiliwa mwaka wa 2024, ambalo halikuidhinishwa na mamlaka ya kitaifa ya ajira.
Ahadi ya kupata uraia wa Urusi
Festus Arasa Omwaba aliwavutia waajiri kupitia shirika lake, Global Face Human Resources Limited. Aliwaahidi watu hao mishahara ya hadi shilingi 350,000 za Kenya (takriban euro 2,300 kwa mwezi), pamoja na marupurupu ya hadi shilingi milioni 1 (takriban euro 6,250), utajiri mkubwa nchini Kenya.
Wengi waliamini ahadi ya kupata uraia wa Urusi: walidhani wangeondoka kwa ajili ya kazi za usalama au walinzi, lakini wakajikuta mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine.
Kulingana na ripoti ya mamlaka, zaidi ya Wakenya 1,000 waliondoka nchini humo katika muktadha huu, wakitumia visa vya watalii. Makumi kati yao walilazwa hospitalini na wengine wengi hawajulikani waliko, na angalau kifo kimoja kimethibitishwa.
Mnamo mwezi Septemba 2025, operesheni ya polisi ilifanya kugunduliwa kwa wahamiaji 22 katika nyumba karibu moja na mji wa Nairobi, huku mikataba isiyosainiwa na pasipoti kadhaa zilikamatwa. Wachunguzi wanadai kwamba kiasi kikubwa cha pesa kililipwa na waathiriwa.
Kesi imepangwa kuikilizwa Machi 30
Festus Arasa Omwamba – ambaye inadaiwa alifanya biashara hiyo pamoja na mshirika ambaye pia anashtakiwa katika kesi hii – alikamatwa katika mji wa Moyale, kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka na Ethiopia. Alitoweka baada ya familia kuanza kupinga kutoweka na vifo vya wapendwa wao katika vita vya Ukraine.
Mshukiwa ameomba kuachiliwa mapema. Kes yao imepangwa kusikilizwa Machi 30. Uchunguzi unaendelea katikati ya tuhuma za mtandao ho na athari zake nje ya nchi.