#HABARI: Waziri wa Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, kwa jitihada zake za kutatua migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa usimamizi makini wa DC Mwema umesaidia kudumisha amani na umoja, mambo ambayo ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya hiyo.
Katika mkutano huo, Dkt. Mwigulu amesikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi huku akisisitiza umuhimu wa makundi yote ya kijamii kuishi kwa kuzingatia utii wa sheria.
Ameyataka makundi ya wakulima na wafugaji kuacha chuki na badala yake washirikiane kwa amani, akionya kuwa serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya yeyote atakayevunja taratibu zilizowekwa na kuhatarisha usalama wa raia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.