
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuwasaidia watu wasiojiweza hususan katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili kutimiza ibada ya funga kwa moyo wa huruma.
Rais Mwinyi ameyasema hayo leo Februari 27, 2026, aliposhiriki Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Fatma Bint Mirdas Mosque, Kilimani, Mkoa wa Mjini Magharibi. Amesema ndani ya jamii kuna watu masikini, wajane, mayatima na wenye ulemavu ambao wanastahili msaada zaidi katika kipindi hiki cha mfungo.
Aidha amewaagiza wafanyabiashara kuepuka kupandisha bei za bidhaa za vyakula akibainisha kuwa Ramadhani si wakati wa kutafuta faida kubwa bali wa kuhurumiana na kusaidiana. Amesema kuwa ni busara kwa wafanyabiashara kushusha au kuacha za kawaida badala ya kupandisha bei ili wananchi wote waweze kumudu kununua mahitaji ya futari. SOMA: Maoni:Tunawatakia Ramadhani njema Waislamu