#HABARI: Watumishi kutoka Idara na Vitengo mbalimbali vya Wizara ya Nishati wamepongeza kasi kubwa ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ambao sasa umefikia asilimia 81.

Wakiongozwa na Bi. Mary Kessy mkoani Tanga leo Februari 27, 2026, watumishi hao wamejionea maendeleo ya mradi huo wa kimkakati wenye urefu wa kilometa 1,443 kutoka Hoima, Uganda mpaka Chongoleani, huku wakiridhishwa na namna unavyofungua fursa za ajira na ujuzi kwa Watanzania.

Maendeleo ya ujenzi katika eneo la mradi yanaonyesha mafanikio makubwa, ambapo uchomeleaji wa vipande vya bomba umekamilika kwa asilimia 100.

Msimamizi kutoka TPDC, Mha. Mussa Msafiri, amebainisha kuwa ujenzi wa matenki umefikia asilimia 88, ujenzi wa jeti asilimia 87, huku vituo vya kusukuma na kupunguza msukumo wa mafuta vikiwa vimefikia asilimia 71.6. Kazi hizi zinaendelea kwa kasi ili kuhakikisha miundombinu yote muhimu inakamilika kwa mujibu wa mpango kazi.

Ushiriki wa TPDC katika mradi huu ni sehemu ya mkakati wa Taifa wa kuendeleza sekta ya mafuta na gesi na kuhakikisha rasilimali hizo zinawanufaisha wazawa.

Kupitia mradi wa EACOP, Watanzania wengi wameendelea kunufaika na fursa za zabuni, ajira za moja kwa moja na mafunzo ya kiufundi, jambo ambalo linaimarisha uchumi wa nchi na kuongeza ujuzi wa ndani katika kusimamia miradi mikubwa ya nishati duniani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *