Chanzo cha picha, Vahid Online.
Shirika la habari la Reuters limemnukuu Waziri wa Ulinzi wa Israel akisema Jumamosi kuwa Israel imefanya shambulio la makombora la kuzuia kabla dhidi ya Iran.
Jeshi la Israel lilitangaza kuwa limewasha ving’ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo “kuwaandaa wananchi kwa uwezekano wa kurushwa kwa makombora kuelekea Israel” kama hatua ya kulipiza kisasi.
Wakati huo huo, Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video ya dakika nane kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social na kuthibitisha kuwa Marekani ilihusika katika shambulizi dhidi ya Iran.
Bado tunasikiliza video na maoni kamili ya Trump na tutakuelezea hivi karibuni.