
Muda wa kusoma: Dakika 2
Marekani na Israel wameanza kuishambulia Iran – ni mpango ambao umekuwa ukizungumziwa kwa wiki kadhaa – mpango ambao umekuwa ukizungumziwa kwa wiki kadhaa.
Rais Donald Trump amesema oparesheni hii inalenga kuhakikisha Iran haifanikiwi kuwa na silaha za nyuklia.
”Ninasema usiku wa leo kwamba uhuru wenu umekaribia. Endelea kujikinga. Usiondoke nyumbani kwako. Ni hatari sana nje. Mabomu yatarushwa kila mahali.” alisema Rais Trum katika taarifa baada ya kuthibitisha kuanzishwa kwa operesheni kubwa ya kijeshi nchini Iran.
”Tukimaliza, kuangusha serikali yenu. Itakuwa nafasi yenu kuchukua. Labda hii itakuwa nafasi yako pekee kwa vizazi. Kwa miaka mingi mmeomba usaidizi wa Marekani lakini humkuupata. Hakuna rais aliyekuwa tayari kufanya kile ambacho niko tayari kufanya usiku wa leo. Sasa una rais ambaye anakupa unachotaka. Basi hebu tuone jinsi mnavyojibu.” aliendelea kusema Trump.
”Markani inawaunga mkono kwa nguvu nyingi na. Sasa ni wakati wa kuchukua udhibiti wa hatima yanu na kuachilia mustakabali wenye mafanikio na utukufu ambao uko karibu na wewe kufikia.” alisema.
Iran hata hivyo imekuwa ikisema haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia – wanatekeleza tu haki yao ya msingi ya kuwa na nishati ya nuklia kwa matumizi mengine isipokuwa silaha.
Hapo jana Ijumaa Februari 27, Rais Donald Trump alisema kuwa Marekani haijafanya “uamuzi wa mwisho” kuhusu kuipiga Iran – lakini akaongeza kuwa “hajafurahishwa” na msimamo wao wa wakati wa mazungumzo ya nyuklia.
Trump alisema kuwa Iran “haiko tayari kutupa kile tunachopaswa kuwa nacho”, akisisitiza kwamba Iran “haiwezi kuwa na silaha za nyuklia”.
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Geneva kati ya nchi hizo mbili yalifanyika mwanzoni mwa wiki, huku pande zote zikisema maendeleo yamepatikana katika kufikia makubaliano.
Hapo awali Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz alitangaza “hali dharura” kote Israel.
Ving’ora vilisikika kote nchini Israel mwendo wa 08:15 saa za ndani (06:15 GMT), kuwatahadharisha watu kuhusu tishio la uwezekano wa shambulio la kombora.
Mashambulizi ya Israel yanatokea huku kukiwa na juhudi za kidiplomasia kati ya maafisa wa Marekani na Iran kufikia makubaliano ya kukomesha mpango wa nyuklia wa Iran na kuepusha vita, na mazungumzo yalitarajiwa kuendelea wiki ijayo.
Iran ilifanya makubaliano katika mazungumzo hayo, lakini Rais wa Marekani Donald Trump – ambaye hapo awali alitishia kuishambulia Iran ili kuwashinikiza viongozi wake kukubali makubaliano – alisema jana “hajafurahishwa” na jinsi majadiliano yalivyokuwa yakiendelea.
Marekani imekuwa ikisema kwamba Iran imekataa kuzungumza na kumaliza mpango wa kwa mazungumzo – lakini Iran imekuwa ikizingumza na jumuiya ya kimataifa lakini hata Marekani wenyewe juu ya uendelezwaji wa program Yao ya nuklia
Lakini Trump ameenda mbali na kuwaambia Wananchi wa Iran kwamba saa yao ya ukombozi imekaribia, na kwamba wakiandae kuichukua nchi yao.
Kauli hii inamaanisha kwamba pamoja na kuharibu viwanda na programu ya nuklia, Marekani na Israel wana mpango mwingine wa ziada kuuondoa kabisa utawala wa sasa wa Iran
Trump ametoa sababu nyingi za nia ya kufanya hivi akitoa mifano ya miaka ya 70 na themanini akisema Iran ilivamia ubalozi wao, ukawateka wananchi wao na kuwauwa Wamarekani katika mazingira mbalimbali
Rais Trump ameongeza pia kwamba Iran ndio mfadhili mkubwa wa Ugaidi duniani akisema ndio imewafadhili Hezbollah na Hamas kuweza kutekeleza shambulio kubwa kuwahi kutokea Israel kwa miaka mingi.
Ukisikiliza hotuba ya Trump unaona anajiamini kweli kweli, lakini wapo wanaoonya kwamba Trump atashangazwa na namna vita hii itakuwa ngumu kwake na kugeuka kwa namna ambayo hajaitarajia bado.
Ni mgogoro wa kufuatilia kwa karibu