.

Chanzo cha picha, Ghana’s Foreign Affairs Ministry/Facebook

Takriban
Waghana 55 wameuawa wakipigana vitani nchini Ukraine, huku wengine wawili
wakishikiliwa kama wafungwa wa kivita, waziri wa mambo ya nje wa Ghana amesema.

Katika
safari yake kwenda Kyiv, Samuel Okudzeto Ablakwa alisema kwamba takriban
Waghana 272 wanaaminika kushawishiwa kuingia katika mzozo huo tangu 2022, akirejelea
mamlaka ya Ukraine.

Ablakwa
alielezea takwimu hizo kama “zinazohuzunisha na kutisha,” akisema
Ghana “haiwezi kufumbia macho takwimu hizi za kuvunja moyo”.

Hakusema ni
upande gani ambao Waghana walikuwa wakipigana lakini waziri wa mambo ya nje wa
Ukraine alisema Jumatano kwamba zaidi ya watu 1,700 kutoka nchi 36 barani
Afrika wamesajiliwa kupigania Urusi.

Waghana 55
ndio idadi kubwa zaidi ya majeruhi kutoka nchi moja ya Afrika kuthibitishwa
rasmi katika vita vya Ukraine na Urusi.

Vyombo vya
habari vya ndani nchini Cameroon vimeripoti kwamba raia wake 94 wamekufa katika
mzozo huo, lakini mamlaka hazijatoa maoni yoyote kuhusu takwimu hizi.

Waafrika
Kusini wawili na takriban Mkenya mmoja wamefariki katika mzozo huo.

Ablakawa
alisema takwimu za majeruhi “sio tu idadi, zinawakilisha maisha ya
binadamu, matumaini ya familia nyingi za Ghana na taifa letu”.

Alisema
serikali ya Ghana imejitolea “kufuatilia na kusambaratisha mipango yote ya
usafirishaji watu kwa njia haramu” pamoja na kuanzisha kampeni kali za
uhamasishaji umma ili kuzuia vijana wa nchi hiyo kuingizwa kwenye mzozo huo.

“Hii si
vita yetu na hatuwezi kuruhusu vijana wetu kuwa ngao za kibinadamu kwa
wengine,” aliongeza.

Siku ya
Alhamisi, raia wa Kenya alishtakiwa kwa tuhuma za kuwashawishi vijana wa
kiume kwenda Urusi na ajira za kazi, lakini wakaishia kupigana nchini Ukraine.
Festus Arasa Omwamba alikana mashtaka hayo.

Jumla ya
Wakenya 1,000 wamesajiliwa kupigania Urusi katika vita vyake vya miaka minne
dhidi ya Ukraine, ilisema ripoti kutoka kwa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ya
Kenya (NIS), iliyotolewa wiki iliyopita.

Ubalozi wa
Urusi nchini Kenya umekanusha madai kwamba ulihusika katika kuwasajili watu
kupigana vitani.

Hata hivyo,
ilisema kwamba sheria ya Urusi iliwaruhusu raia wa kigeni waliopo nchini humo
kisheria kujiunga na jeshi kwa hiari.

Siku ya
Jumatano, waziri wa mambo ya nje wa Ghana alimhimiza Rais Volodymyr Zelensky
kuwaachilia huru wafungwa wawili wa kivita wa Ghana waliokamatwa wakipigania
Urusi.

“Wao ni
waathiriwa wa udanganyifu, taarifa za uongo, taarifa potofu, na mitandao ya
biashara haramu ya wahalifu,” alisema.

Aliishukuru
Ukraine kwa kuhakikisha sheria za kimataifa zinaheshimiwa katika
kuwashughulikia wafungwa.

“Tumepokea
ripoti kwamba wako katika afya njema,” alisema. “Hawajateswa.
Hawajatendewa ukatili tangu walipokamatwa.”

Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiga alisema pande zote mbili zilijadili “kwa uwazi” kuhusu uwezekano wa kuwarudisha wafungwa hao Ghana.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *