
Suala la ndege iliyotelekezwa kwa karibu miaka ishirini kwenye lami ya uwanja wa ndege wa Faro nchini Ureno limeibuka tena. Mamlaka ya uwanja wa ndege wa Ureno imetoa notisi rasmi kwa Jean-Pierre Bemba, Naibu Waziri Mkuu wa Uchukuzi wa Kongo wa sasa, ikitaka aje achukuwe ndege aina ya Boeing 727, ambayo ni mali yake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ndege hiyo inazuiliwa kwenye uwanja huo tangu mwaka 2007, mwaka ambao ilikamatwa kwa ombi la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Jean-Pierre Bemba sasa ana siku 60 za kuiondoa ndege hiyo.
Kama sehemu ya kesi dhidi ya Jean-Pierre Bemba mbele ya ICC, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka iliomba nchi kadhaa kutambua, kupata, kuzuia, na kunyakua mali zake. Ilikuwa katika muktadha huu kwamba Boeing 727-100, iliyoegeshwa huko Faro, ilikamatwa na mamlaka ya Ureno. Ndege hiyo ilibaki hapo kwa miaka 19, bila kuruka.
Kilichobadilika ni sheria ya Ureno. Mnamo mwezi Machi 2025, Ureno ilipitisha sheria ya amri inayoanzisha mfumo mpya wa ndege zilizotelekezwa katika viwanja vya ndege. Ndege sasa inaweza kuchukuliwa kuwa imeegeshwa kinyume cha sheria baada ya siku 90. Mmiliki anaarifiwa kuiondoa. Ikiwa atashindwa kufanya hivyo, ndege inaweza kutangazwa kuwa imetelekezwa, kisha kutaifishwa na serikali, kuuzwa au kuharibiwa. Ni kwa msingi huu kwamba mamlaka ya uwanja wa ndege imetoa notisi rasmi kwa Jean-Pierre Bemba.
Jean-Pierre Bemba amekataa ksema chochote
Gharama ya kinadharia ya maegesho inafikia karibu euro milioni moja kwa zaidi ya miaka 19. Jean-Pierre Bemba alikataa kutoa kusema chochote. Lakini washirika wake wanaibua hoja ya kisheria. Wanadai kwamba ICC ndiyo iliyoamuru ndege izuiliwe. Kwa hivyo, ni jukumu la ICC kutoa agizo hili kwa mamlaka ya uwanja wa ndege wa Ureno. Na ikiwa ni lazima, wanasema, ni ICC inapaswa kulipa gharama hiyo, sio Jean-Pierre Bemba.