
Sheria kuhusu mashirika yasiyo ya kiserikali imeanza kutumika siku ya Jumanne, Machi 3, nchini Angola, baada ya kupitishwa na Bunge linalodhibitiwa kwa kiasi kikubwa na chama tawala, MPLA. Sheria hii inaunda chombo cha utawala ambacho wanachama wake huteuliwa moja kwa moja na rais Joao Lourenço, waliopewa jukumu la “kufuatilia” shughuli na ufadhili wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wasiwasi unaongezeka miongoni mwa mashirika ya kiraia, ambayo yanaona kama “kuingiliwa kwa serikali” katika kuelekea uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi Agosti 2027
Mswada huu wa sheria unaeleza wazi kwamba lengo la sheria kuhusu mashirika ya kiraia ni kupambana na utakatishaji fedha na ufadhili wa ugaidi. Mwanaharakati Pedro Ngonga, mkuu wa shirika lisilo lakiserikali lenye makao yake makuu Luanda, anasema “ana shida kuelewa” hoja hii. “Hakujawahi kuwa na shirika linaloshutumiwa au kushtakiwa kwa utakatishaji fedha au ugaidi,” anasema. Huu ni mkakati tu wa kujiandaa kwa uchaguzi wa mwaka 2027. Sheria hii inadhoofisha mashirika yasiyo ya kiserikali, ambayo hayataweza kutoa tahadhari kuhusu kasoro zinazoweza kutokea katika mchakato wa uchaguzi,” anabainisha.
Sheria hiyo awali ilichukuliwa kuwa kinyume na katiba na Mahakama Kuu ya Angola kabla ya kufutwa na kisha kuidhinishwa. Kuanzia sasa, mashirika yasiyo ya kiserikali yatawasilisha ripoti za mara kwa mara kuhusu shughuli na ufadhili wao. Chombo hicho kilichoteuliwa na rais kitakuwa na jukumu la kuidhinisha, au kukataa, ripoti hizi.
Wito wa kuandamana Machi 14
“Fikiria ninapopata ufadhili wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari. Inatosha tu chombo hiki kukataa faili hii. Katika hali ya kawaida, tunawajibika kwa wafadhili wetu, si kwa serikali. Na kwa sasa, tutalazimika kusitisha shughuli zetu,” anaelezea Pedro Ngonga.
Sheria hii pia inatumika kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kigeni yanayofanya kazi nchini Angola. Mashirika ya kiraia yameitisha maandamano Machi 14 na chama cha wanasheria kinataka kupinga sheria hiyo mahakamani.