Nchini Afrika, zaidi ya nchi ishirini zimesaini makubaliano ya pande mbili na Marekani kama sehemu ya “Mkakati wa Afya wa Kimataifa wa – America First.” Programu hii, iliyozinduliwa na utawala wa Trump, inalenga rasmi “kulinda eneo la kitaifa kwa kuzuia milipuko ya magonjwa ya kuambukiza kufikia ufuo wa Amerika […] na kuokoa mamilioni ya maisha na kusaidia nchi kupunguza utegemezi wao kwa misaada ya kigeni.” Lakini baadhi ya nchi za Afrika yameamua kutofuata masharti ya Marekani.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès

Kufuatia marekebisho na kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa programu kadhaa za afya za Marekani, nchi zilizonufaika nazo sasa zinashinikizwa kukubali makubaliano ya pande mbili na utawala wa Trump ili kufungua misaada mipya.

Katika bara la Afrika, nchi nyingi tayari zimekubali kushiriki kwa kufuata sheria za mkakati huu wa “America First “, kusaini mikataba yenye thamani ya mamilioni ya euro. Marekani imesaini makubaliano ya pande mbili ya miaka mitano na zaidi ya nchi ishirini za Afrika, ikiwa ni pamoja na, hivi karibuni, Burkina Faso, Niger, na DRC.

Kulingana na Washington, lengo la muda mrefu ni kupunguza utegemezi wa misaada ya kimataifa, na nchi husika zinajitolea katika programu za ufadhili wa pamoja, kwa mfano, kupambana na malaria, VVU, na vifo vya akina mama na watoto wachanga.

“Chombo cha mazungumzo tu kwa utawala usijali ya nchi zigine”

Pia ni muktadha wa kimataifa unaosukuma nchi hizi kukubali masharti ya Marekani, kwani ufadhili unazidi kuwa mdogo. Ufaransa, kwa mfano, inatarajiwa kupunguza kwa 58% kiasi ambacho imetenga kwa Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Lakini kwa Asia Russell, mkurugenzi wa Health Gap, shirika linalopigania upatikanaji bora wa matibabu ya VVU na UKIMWI, anasema inatia wasiwasi sana kuona mikataba kama hiyo ikisainiwa bila kushauriana. “Mikataba hii ya pande mbili ni tofauti sana na jinsi mpango wa PEPFAR [President’s Emergency Plan for AIDS Relief, mpango wa msaada wa dharura wa mapambano dhidi ya UKIMWI nje ya nchi uliozinduliwa mwaka 2003 na Marekani] ulivyofanya kazi,” anaelezea. “Ilitokana na ushahidi wa kisayansi, kwa uwazi kamili, huku serikali mbalimbali zikishirikiana na watu wanaoishi na VVU na serikali ya Marekani ili kutathmini maendeleo ya programu na kubaini ni wapi mabilioni ya dola yanapaswa kuwekezwa, katika kliniki zipi, na katika maeneo gani.” »

Anasikitika: “Wakati afya inakuwa njia tu ya kujadiliana kwa utawala usiojali mslahi ya nchi zingine, unaotaka, badala yake, kutumia rasilimali za matiafa huru, kama vile madini, inaweza kusababisha matokeo mabaya. Programu zinaweza kushindwa kukidhi mahitaji ya watu waliohatairini kupoteza maisha ikiwa hawana matibabu au njia bora za kuzuia.”

Kukosekana kwa uwazi

Kwa kweli, vifungu na kiasi hutofautiana, kulingana na mazungumzo ambayo yamefanyika. Lakini, kwa ujumla, kuna uwazi mdogo sana, hasa kuhusu kushiriki data ya afya, ambayo inaweza kuipa Marekani fursa katika ufuatiliaji wa afya.

Hili ndilo lililosababisha Zimbabwe kukataa kusaini makubaliano kama hayo, “ambayo si kwa maslahi yetu,” kulingana na msemaji wa serikali.

Zambia, kwa upande wake, inaomba kujadiliwa upya, huku baadhi ya dalili zikionyesha kwamba makubaliano yangehitajika katika sekta ya madini. Kuhusu Kenya, ni mfumo wa haki uliozuia kwa muda utekelezaji wa maandishi yaliyosainiwa, ili kuthibitisha kwamba yanafuata sheria za ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *