
Siku chache baada ya kutangaza kuliwekea vikwazo jeshi la Rwanda pamoja na maofisa wake wa juu wa kijeshi, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, amesema nchi yake haitatoa viza za kuingia nchini humo kwa maofisa wa Kigali, kutokana na kuhusika kwao kwenye mzozo wa DRC.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake, Rubio amesema maofisa wote wanaohusika, kushiriki moja kwa moja au vinginevyo, katika kuzuia mchakato wa kupata amani ya kudumu kwenye eneo la maziwa makuu, watakabiliwa na vikwazo.
Juma lililopita, Marekani ilidai jeshi la Rwanda limeendelea kuwasaidia waasi wa M23 kutatiza usalama mashariki mwa Congo, licha ya nchi hiyo kutia saini makubaliano ya Washington mwishoni mwa mwaka jana.
Je vikwazo vya Marekani dhidi ya Rwanda vitakuwa na athari gani?
Tangazo hili la Marekani, linakuja wakati huu Kinshasa ikiendelea kutafuta uungwaji mkono wa Jumuiya ya kimataifa, ambapo imekuwa ikiituhumu Rwanda kuendelea kushirikiana na waasi hao