.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baraza la
Wataalamu la Iran limemchagua Mojtaba Khamenei kuchukua nafasi ya baba yake,
Ayatollah Ali Khamenei, kama kiongozi mkuu mpya wa nchi hiyo, vyombo vya habari
vya serikali vinaripoti.

Jinsi
uteuzi wa Khamenei ulivyotangazwa

Taarifa
kutoka kwa Bunge la Wataalamu ilisomwa kwa sauti na mtangazaji kwenye Televisheni
ya serikali:

“Licha
ya hali mbaya ya wakati wa vita na vitisho vya moja kwa moja vya maadui dhidi
ya taasisi hii maarufu, na licha ya kulipuliwa kwa ofisi za Sekretarieti ya
Baraza la Wataalamu, na kusababisha vifo vya wafanyakazi kadhaa na wanachama wa
timu yake ya usalama, hawakusita hata kidogo katika mchakato wa kumchagua na
kuanzisha uongozi wa mfumo wa Kiislamu.”

Mtangazaji alipaza
sauti “Allahu Akbar, Allahu Akbar, Khamenei ndiye kiongozi.”

Kiongozi mpya aliyechaguliwa licha ya vitisho – Mkuu wa
Usalama wa Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran
amelishukuru Baraza la Wataalamu kwa kumchagua mrithi wa Ali Khamenei licha ya “tishio la Trump kulishambulia kwa bomu”, kulingana na mashirika
mengi ya habari ya Iran.

Ali Larijani anasema “maadui” wa Tehran
walidhani nchi “itakuwa katika hali ya mkwamo” kufuatia kifo cha Ali
Khamenei lakini hatimaye Bunge limeendelea na uteuzi wa Mojtaba Khamenei.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *