Wanasiasa wa Iran wanaoishi nje ya nchi pamoja na watetezi wa haki za binadamu, sasa wanazitaka mamlaka za Australia, kuwapa hifadhi wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mtoto wa kiongozi wa zamani wa Iran, Reza Pahlavi, amesema ikiwa Australia itakataa kutoa hifadhi kwa wachezaji hao, huenda wakakabiliwa na hali mbaya watakaporejea nyumbani.

Reza ametoa wito huo, baada ya hapo jana timu ya wanawake ya Iran, kuaga rasmi mashindano ya Kombe la Mataifa ya Asia, ambapo wachezaji hao waliimba wimbo wao wa taifa.

“Wachezaji wa timu ya taifa ya Iran wako katika shinikizo kubwa pamoja na vitisho toka kwa utawala wa kiislamu”, alinukuliwa Reza kupitia mtandao wake wa kijamii.

Wakati michuano hiyo ikianza wiki moja iliyopita, wachezaji hao waligoma kuimba wimbo wa taifa, katika kile kilichotafsiriwa kama kupinga utawala wa sasa ambao uko kwenye shinikizo toka kwa Marekani na Israel.

Mbali na Reza, yako pia mashirika ya kutetea haki za binadamu akiwemo mwanaharakati mkongwe, JK Rowling.

Hivi majuzi mtangazaji wa televisheni ya taifa, aliwataja wachezaji hao kama wasaliti kwa kutoimba wimbo wa taifa.

Mashabiki kwenye michuano hii, walikuwa wakiimba nyimbo kutaka mabadiliko ya uongozi nchini Iran, ambapo baada ya mchezo walizingira basi la timu ya Iran wakisema wanataka wasichana hao wawekwe huru.

Hata hivyo licha ya wito huu, serikali ya Canberra, haijatoa kauli yoyote ikiwa iko tayari kutoa hifadhi ya ukimbizi kwa wachezaji hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *