
Nchini Afrika Kusini, kama ilivyo katika nchi nyingi duniani kote, kuna wasiwasi kuhusu athari za kiuchumi za vita katika Mashariki ya Kati, ikizingatiwa kwamba Pretoria inaagiza sehemu kubwa ya mafuta yake. Hadi sasa, Afrika Kusini imekuwa ikifurahia kasi ya kiuchumi yenye kutia moyo na ilikuwa imeweka bajeti yake ya mwaka 2026 kwenye ishara hizi chanya. Vita vimebadilisha kila kitu: athari kuu kwa wanunuzi wa Afrika Kusini ni ongezeko la bei ya mafuta.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu nchini Afrika Kusini, Valentin Hugues
Benki kuu ya Afrika Kusini imetangaza kuwa inarekebisha mipango yake. Gavana wa Benki kuu ya afrika Kusini anaeleza kwamba kwa bei ya sasa ya pipa la mafuta, zaidi ya dola 90, hata matumaini yao waliokuwa nayo mwezi Januari mwaka huu hayana nafasi tena.
“Sasa tumekuwa waathiriwa wa migogoro inayotokea mbali na nyumbani,” ametangaza Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, kabla ya kutaja ongezeko kubwa la gharama za nishati katika bara zima.
Hali tete
Mchumi Khutso Makua anaongeza kuwa vita hivyo vinaondoa matumaini yote ya kiuchumi ya Afrika Kusini. Hadi sasa, mfumuko wa bei kwa ujumla ulikuwa wa wastani. Mnamo mwezi Januari 2026, bei ya lita moja ya mafuta ilikuwa imefikia kiwango chake cha chini kabisa tangu miaka minne iliyopita.
Hata hivyo, kutokana na vita Mashariki ya Kati, Afrika Kusini tayari imetekeleza ongezeko la bei ya mafuta kwa Waafrika Kusini. Hali nyingine nzito kwa Afrika Kusini: hadi hivi karibuni, randi ya Afrika Kusini ilikuwa imeimarika sana dhidi ya dola, kutokana na mauzo yake ya mafuta. Leo, hali imebadilika, na sarafu ya Afrika Kusini inapoteza tahamani.