Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeshambulia miundombinu muhimu katika kambi nne za Marekani huko Kuwait na Bahrain katika awamu ya kwanza ya majibu yake dhidi ya ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita unaofanywa na Marekani.

Taarifa iliyotolewa na IRGC imesema, vituo na kambi za kijeshi za Marekani zilizolengwa ni pamoja na Arifjan na Ali Al Salem huko Kuwait na Juffair na Sheikh Isa huko Bahrain, na kueleza kwamba vituo hivyo vimepigwa kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani.

Kauli hiyo imetolewa baada ya ndege za Marekani kufanya mashambulizi katika maeneo kadhaa ya kusini mwa Iran, zikilenga miundombinu ya raia na kuua mtu mmoja, mbali na kushambulia daraja katika jimbo la kaskazini la Golestan.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) “limelionya jeshi la Marekani linaloua watoto kwamba iwapo litarudia vitendo vyake vya uchokozi, majibu yetu yatapanuliwa zaidi na kujumuisha kambi zingine za Marekani katika eneo lote la Asia Magharibi.”

Wakati huo huo, IRGC imeutaja uchokozi huo mpya wa Marekani kuwa yametokana na hamaki ya “haraka” wa Marekani kwa mahudhurio makubwa wananchi katika nchi jirani ya Iraq kwenye shughuli ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

“Msafara huu mkubwa wa mazishi, umewatia wahka watawala maghururi wa Marekani na kuwalazimisha kujibu haraka onyesho hili la nguvu za umma,” taarifa hiyo imesema.

Taarifa hiyo imeongeza kwamba: Washington, ilikuwa na nia “kufunika habari za tukio hilo la ajabu lisilo na kifani na kuficha tukio hili la kutia matumaini mbele ya macho ya walimwengu.”

Taarifa ya IRGC imeongeza kwamba, hata hivyo, “hawajui ukweli kwamba uhalifu huu utawaamsha zaidi watu wa dunia na kuimarisha azma yao ya kuwa na nafasi katika mapambano dhidi ya ‘Shetani Mkuu,’ yaani Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *