
Bunge la Lebanon limetangaza kuahirisha uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika mwezi Mei kwa miaka miwili kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israel na Hezbollah inayounga mkono Iran, kulingana na taarifa kutoka kwa rais wake, Nabih Berri.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Bunge la Lebanon limeahirishaleo Jumatatu uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanyika Mei 2026 kwa miaka miwili kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Israeli na Hezbollah inayounga mkono Iran, kulingana na taarifa kutoka kwa rais wake, Nabih Berri, iliyonukuliwa na shirika la habari la AFP.
Bunge limekutana na wanachama wa Hezbollah wameshiriki mkutano huo, huku ndege za Israel zikishambulia vitongoji vya kusini vilivyo karibu, ngome ya Hezbollah.
Shambulio jipya la Israel kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya Hezbollah
Jeshi la anga la Israel lilifanya shambulio lingine siku ya Jumatatu asubuhi kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya Hezbollah, kulingana na shirika la habari la serikali INA na picha za AFPTV. Msemaji wa jeshi la Israel anayezungumza Kiarabu alionya kwamba lililenga matawi ya kampuni ya kifedha ya Al-Qard Al-Hassan, yenye uhusiano na Hezbollah, iliyowekwa katika ngome za kundi hilo.