Mjadala kuhusu marekebisho ya katiba umeibuka tena nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu chama cha UDPS,  kiliyo madarakani tangu mwaka 2019, kilipotangaza nia yake ya kurekebisha Katiba, hali ambayo itamuwezesha rais Félix Tshisekedi kugombea muhula wa tatu. Kwa sasa anajianda kuondoka madarakani mwaka wa 2028. Makamu wa pili wa rais wa Baraza la Seneti, Modeste Bahati, amepinga hadharani uwezekano huu, kama vile upinzani, ambao umesema hautokubali.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Pascal Mulegwa

Kulingana na baadhi ya wanasiasa kutoka serikalini, Félix Tshisekedi hatekelezi mamlaka, bali kazi.. Wengine wanapendekeza kwamba kusiwe na uchaguzi tena hadi ghasia mashariki mwa nchi zitakapoisha.

Siku ya Jumamosi, Machi 7, mkuu wa chama tawala cha UDPS, Augustin Kabuya, aliwapa nafasi maafisa wa chama na wanaharakati waliokusanyika makao makuu: “Mobutu alirekebisha Katiba mara 17, Laurent-Désiré Kabila aliirekebisha mara tatu, na Joseph Kabila akairekebisha mara moja. Kwa misingi gani mtazuia utawala wetu kuifanyia marekebisho? Tuwe wazi, tutaifanyia marekebisho Katiba hii.”

“Hatua itakayoleta madhara makubwa kwa nchi” 

Siku hiyo, Waziri wa Michezo Didier Budimbu, mshirika wa rais, alisisitiza hoja hiyo katika mkutano wa hadhara nje kidogo ya mji wa Kinshasa: “Tusijifanye wajinga. Hatutajifanya kwamba mihula hiyo miwili inaisha kisha tunakabidhi madaraka, kwa nani? Na mtu tunayempa afanye nini na madaraka hayo? Tunaelekea moja kwa moja kwa muhula wa tatu, na hatutaona aibu.” “‘Hatua hii italeta madhara makubwa kwa nchi hii,’ inaonya kambi ya rais wa zamani Joseph Kabila, ambayo inabainisha kwamba utawala wa sasa unataka ‘kwenda kinyume na matakwa ya raia.’ Kiongozi wa upinzani Martin Fayulu tayari ameona mjadala huo kuwa ‘haufai,’ akitaka ‘watu kutopumbazwa tena.’ Kwa upande wake, Jean-Marc Kabund anasema mjadala huo ‘haukubaliki kimaadili’ na ‘hauwajibiki kisiasa’ katikati ya mgogoro unaoendelea mashariki mwa nchi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *