Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, limeipa nchi ya Rwanda haki ya kuwa mwenyeji wa michuano minne ya ukanda katika kalenda yam waka 2026.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi mtendaji wa muda wa CECAFA, Jean Sseninde, amthibitisha kuwa Rwanda na Tanzania kwa pamoja zitaandaa mashindano 6 ya ukanda yaliyopangwa kwa msimu wa 2026.

Nchi ya Rwanda, sasa itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la Kagame mjini Kigali kuanzia Julai 18 hadi Agosti 9.

Mwaka uliopita timu ya Tanzania, SIngida Black Stars walitawazwa kuwa mabingwa wa michuano ya Kagame, baada ya kuwafunga Al Hilal kwenye mchezo wa fainali.

Mbali na kombe la Kagame, Rwanda pia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya shule za sekondari yanayoratibiwa na CAF, mechi za kufuzu klabu bingwa Afrika na zile za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17.

Tanzania kwa upande wake, yenyewe itaandaa fainali za wasichana chini ya umri wa miaka 17 kwenye ukanda wa CECAFA kuanzia Mei 30 hadi Juni 14, kabla ya kuandaa mechi za kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kuanzia Septemba 12 hadi 27.

Nchi wanachama za CECAFA zinajumuisha Rwanda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda na Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *