Kipato kidogo kwa wananchi hasa wa vijijini kimesababisha kupunguza kasi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwamo gesi.

Hali hiyo inachangia baadhi ya wananchi ushindwa kujaza mitungi yao pindi inapokwisha na kujikuta wakirudia matumizi ya mkaa na kuni.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam leo wakati wa mafunzo maalum ya masuala ya
mazingira kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari wanawake kutoka vyombo
mbalimbali vya habari nchini.

Meneja wa Uhusiano na Masoko wa kampuni ya Taifa Gas, Oscar Shalukindo, amesema
licha ya jitihada zinazofanywa za kusogeza huduma karibu na wananchi ya upatikanaji wa
gesi bado baadhi yao hupata ugumu wa kujaza mitungi yao pindi gesi inapokwisha.

“Taasisi mbalimbali zimekuwa zikigawa mitungi ya gesi bure, lakn punde inapoisha watumiaji wake wanashindwa kujaza tena kutoka na hali ya maisha,” amesema
Shelukindo.

Kwa mujibu wa Shelukindo, takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji wa gesi hawazidi asilimia 10 mpaka sasa jambo linaloashiria kuwa bado wanatumia nishati zenye madhara ikiwamo mkaa na kuni.

Naye Mratibu wa Mradi wa Taasisi ya Mazingira, Ibrahimu Haule, amesema mafunzo hayo
yamelenga kuwapa waandishi wanawake maarifa yatakayowawezesha kuandika kwa ufanisi
kuhusu habari za mazingira ili watumie elimu hiyo kuelikisha jami.
#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *