Jeshi la Sudan Kusini, limetangaza kuuchukua tena Mji wa kimkakati wa Akobo ulioko kaskazini mwa jimbo la Jonglei  kutoka kwa wapiganaji wa upinzani baada ya kuanzisha mashambulio yake ya wiki hii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Lul Ruai Koang, msemaji wa jeshi, Mji huo ulioko kwenye mpaka kati yake na Ethiopia, ulichukuliwa na vikosi vya serikali baada ya kuwaondoa wapiganaji wa (SPLA-IO).

Kabla ya kuuchukua Mji huo siku ya Jumanne, jeshi lilidai zaidi wa wapiganaji 50 walikuwa wameuawa, magari yao saba yaliokuwa yamebeba silaha nzito yakichukuliwa.

Aidha limethibitisha kwamba wanajeshi wake 13-waliuawa kwenye mapigano na vikosi vya upinzani wakati wengine 20 wakijeruhiwa.

Mapema wiki hii serikali ya Juba iliagiza raia kwenyue mji huo pamoja na wafanyikazi wa mashirika ya misaada wakiwemo wale wa Umoja wa mataifa kuondoka kabla ya operesheni yake.

Baada ya kuchukua tena udhibiti wa Mji huo, Wanajeshi wa serikali wamewataka wafanyikazi wa mashirika ya misaada kurejelea huduma zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *