Wabunge nchini Senegal wamepitisha sheria siku ya Jumatano, Machi 11, inayoongeza adhabu kwa mahusiano ya ngono ya wapenzi wa jinsia moja. Marekebisho ya Ibara ya 19 ya kanuni ya adhabu yanaongeza maradufu adhabu za kifungo kwa vitendo vya ushoga.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Wakati wimbi la kukamatwa kwa watu wanaoshutumiwa kwa madai ya ushoga likiendelea nchini Senegal, sheria hii mpya inapendekeza kuongeza adhabu za kifungo kutoka miaka mitano hadi kumi, ikilinganishwa na mwaka mmoja wa sasa hadi miaka mitano, kwa yeyote anayepatikana na hatia ya vitendo vinavyoitwa “visivyo vya kawaida”. Sheria hii pia inatoza faini iliyoongezwa, ambayo inaweza kufikia faranga za CFA milioni 10, ikilinganishwa na milioni 1.5 pekee kwa sasa.

Rasimu hii mpya pia inafafanua dhana ya “vitendo visivyo vya kawaida” kujumuisha “vitendo vya ngono kati ya watu wawili wa jinsia moja.” Makosa mawili mapya pia yamejumuishwa katika sheria hii: kutukuzwa na kufadhili ushoga, kosa ambalo linaadhibiwa kwa kifungo cha miaka mitatu hadi saba jela.

Mijadala hii inavutia umati mkubwa wa watu. Siku ya kupiga kura, Jumatano, Machi 11, chumba cha mahakama kilikuwa kimejaa watu. Hakuna hata mmoja aliyesikika akitaka ushoga uondolewe kisheria au hukumu nyepesi zaidi.

Upinzani unaikosoa serikali kwa kutochuka hatua kali zaidi, na haswa kwa kutotimiza ahadi yake ya kufanya ushoga kuwa uhalifu, badala ya kosa dogo.

Kwa Mbunge wa PASTEF Ismaël Wone, kurekebisha sheria hii ya mwaka 1965 ilikuwa ahadi ya kampeni. “Kwa miaka miwili, watu wamekuwa wakitushinikiza, wakisema, ‘Mliahidi kufuta sheria hii kuhusu ushoga.’ Ilibidi ifanyike,” alisema, akiongeza kwamba, kwa maoni yake, ushoga unaenda “kinyume na maadili yetu na mila zetu.”

Mbunge huru Thierno Alassane Sall, kwa upande wake, anabaini kwamba mjadala huu unaondoa mawazo kutoka kwa matatizo mengine. Kulingana naye, katika muktadha mgumu wa kiuchumi na kijamii, kupendekeza sheria kandamizi zaidi kunawaruhusu “kuhamasisha umma kuhusu mjadala wa kijamii ambao haushughulikii matatizo, mgogoro mkubwa, na wasiwasi unaowakumba raia wa Senegal.”

Nakal hii ilipitishwa na Bunge la taifa liinaloongozwa na chama tawala. PASTEF inashikilia viti 109 kati ya 165 Bungeni.

Ingawa sheria hiyo bado inahitaji kutangazwa na Rais Bassirou Diomaye Faye ili ianze kutumika, mashirika ya haki za binadamu tayari yanahofia kwamba itachochea hali ya chuki dhidi ya watu wa jinsia moja nchini.

Mtazamo huu unashirikiwa na mwandishi wa riwaya na mwanaharakati Ndeye Fatou Kane, ambaye anabaini kwamba Senegal imekuwa ikichukua mwelekeo wa kutia wasiwasi katika miaka ya hivi karibuni. “Hata kabla ya kujadili masuala ya ushoga na LGBT, hakuna tena dhana yoyote ya masha ya mtu binafsi [nchini]. Na tutathibitishaje mwelekeo wa kijinsia wa mtu? Nimeona video ambazo raia walichukua sheria mikononi mwao kwa sababu tu walimtuhumu mtu kwa kuwa mke au kuonyesha tabia za kike kwa kuwa shoga,” anasema kwa hasira, kabla ya kuendelea: “Wakati mashoga, au watu wanaodhaniwa kuwa mashoga, wanaposhiriki katika kile wanachokiita shughuli ‘zisizo za kawaida’, je, wako hata hadharani?” […] Kwa sasa kuna Uislamu nchini Senegal ambao unamaanisha kwamba chochote chenye maana za Magharibi kinakataliwa rasmi. Na hicho ndicho kilicho hatari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *