Raia nchini Jamhuri ya Congo wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, katika uchaguzi ambao rais Denis Sassou nguesso mwenye umri wa miaka 82 anapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Sassou Nguesso ambaye ameongoza taifa hilo  tangu 1979, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wengine sita wenye umaarufu mdogo, baada ya vyama vikuu vya upinzani kuchukua maamuzi ya kutokuwa na wagombea katika uchaguzi huo.

Wapinzani wakuu wawili wa upinzani Jenerali Jean-Marie michel makoko na Andre Okombi Salissa, wanazuiliwa gerezani  kwa karibu muongo mmoja baada ya kushtakiwa na makosa ya kuhatarisha usalama wa taifa.

Hata hivyo uchgauzi huo unakwenda kufanyika katika mazingira ya hofu ambayo makundi ya haki za binadamu  yanasema yametokana na ukandamizaji dhidi ya wapinzani.

Mgombea wa upinzani Uphrem Dave Mafoula katikamkutano wake wa hadhara jijini Brazaville juma hili, alitoa wito kwa wafuasi wake kuchagua kiongozi mbadala.

Zaidi wa raia wa nchi hiyo milioni 3.2 wamesajiliwa kama wapiga kura, hata hivyo wengi wao wanasema hawatashiriki zoezi hilo, wakisema hawatarajii kushtushwa na matokeo ya uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *