MWANAUME DEPU, DAIMA MBELE

YANGA ileee, Maria Depu mwanaume wa shoka analibeba chama mabegani. Goli la dhahabu dakika za jioni, linaipa timu pointi zote tatu mbele Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu NBC.

Technically ya Prisons ambayo imetoka kuzunguka barabarani zaidi ya kilometaa 100, lakini bado wamekuwa solid kiasi kile mpaka dakika 79 kuruhusu goli. Maana haliisi ya focus & commitment. “Ishatokea acha kipigwe”.

‎Prisons kwenye mpango kazi mama wa ku defend wamekuwa bora sana. Bahati mbaya kwao wakakosa uharaka wa kuondoka kutafuta goli nyakati ambazo Yanga yote ilikuwa kwenye zone yao. Mipira yote wameitupa juu kirahisi.

‎Wajela Wangekuwa Smart kwenye counter attack kuna kila dalili ingewalipa.

‎Nimependa zile mbinu za makocha wote wawili. Wakati Nsajigwa anamtoa winga Chanongo anamuingiza defensive midfielder Masoud Cabaye. Lengo kudefend more, ndio wakati Pedro kamnyanyua Depu kuchukua nafasi ya Damaro. Lengo attack more. Tactical Sub.

‎Max Nzengeli What A Performance.Kuna time mwamba leo kaupitisha mpira guu la kushoto na kutii amri.

‎Faul ambayo imezaa goli. Beki wa Prisons kacheza mpira na sio miguu ya mchezaji wa Yanga. Wrong decision. Mbissa akaharibu zaidi, punch gani ile dakika zile tena mbele ya teka. Still Depu anabaki shujaa kunusa hatari.

‎Line 2. Dakika 51 kazima shambulizi la Prisons kimakosa. Bacca kajichanua makusudi kumblock Chanongo. Ilipaswa kuwa faul.

‎Yule beki Mkenya wa Prisons mtu sana. Timing ya maana kuondosha hatari. Amekuwa na mechi nzuri sana.

‎Full Time

Prisons 0-1Yanga

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *