Maseneta Elizabeth Warren na Chriss Van Hollen wa Marekani wametoa wito wa kutimuliwa Waziri wa Vita wa nchi hiyo, Pete Hegseth, kwa sababu ya kutenda jinai ya kuua watoto wadogo wa shule ya msingi nchini Iran.

Elizabeth Warren na Chriss Van Hollen wamesema kuwa Waziri wa Vita wa Marekani, Pete Hegseth anapaswa kufukuzwa kwa sababu ya kushambulia shule ya msingi wa watoto wa kike ya Minab, kusini mwa Iran.

Ripoti zinasema, Seneta Elizabeth Warren ametangaza kuwa uchunguzi wa awali wa Wizara ya Vita ya Marekani, Pentagon, unaonyesha kuwa Washington ndiyo iliyofanya shambulizi lililolenga shule hiyo ya wasichana nchini Iran.

Seneta Chriss Van Hollen pia ametangaza kuwa, Pete Hegseth amehatarisha maisha na wanajeshi wa Marekani kwa kuweka wazi mipango ya siri ya mashambulizi Marekani dhidi ya Iran katika mtandao wa kijamii wa Signal.

Pete Hegseth akiwa pamoja na Trump

Seneta huyo ameongeza kuwa, Waziri wa Vita wa Marekani pia amefanya jinai ya kivita kwa kushiriki katika kushambulia boti za raia katika Bahari ya Karibi.

Kabla ya hapo, Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Elimu Duniani, Gordon Brown alikuwa ametoa wito wa kufuatiliwa kisheria wale waliohusika na mauaji ya wanafunzi wa shule ya wasichana ya Minab nchini Iran na kusema: Shambulizi dhidi ya shule ya msingi ya Minab limeonyesha kuwa, shule na wanafunzi sasa zimekuwa shabaha ya mashambulizi.

Gordon Brown, amesema watoto hawapasi kufanywa wahanga wa vita, na shule na hospitali hazipaswi kushambuliwa.

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ameongeza kuwa, “shule ambazo zinapaswa kuwa kimbilio salama la wanafunzi zimegeuka na kuwa makaburi yao.” 

Tarehe 28 Februari serikali ya Marekani ilikiuka sheria zote za kimataifa na kushambulia shule ya Msingi ya watoto wa kike ya Minab katika mkoa wa Hormuzgan (kusini mwa Iran) ambapo wanafunzi karibu 170 wa kike na walimu 20 wa shule hiyo waliuawa shahidi na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *