‎#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa, amewaasa waumini wa dini ya Kiislamu kuwalea watoto katika misingi ya kumcha Mungu ili kuwakinga na matendo maovu.

Akizungumza katika mashindano ya kusoma Qur’an yaliyofanyika Kata ya Buyuni, Silaa amesisitiza kuwa malezi yenye imani ni nguzo muhimu katika kujenga taifa bora lenye kizazi chenye hofu ya Mungu na maadili mema.

Mashindano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Silaa aliyoitoa mwaka jana kwa lengo la kuhamasisha vijana kujifunza na kuhifadhi Qur’an Tukufu. Katika hafla hiyo, washindi na washiriki mbalimbali walizawadiwa zawadi kama hamasa, huku mwanzilishi huyo akibainisha kuwa mashindano hayo yatakuwa endelevu ili kukuza vipaji na elimu ya dini kwa vijana wa Ukonga.

Kwa upande wake, Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ilala amempongeza Jerry Silaa kwa juhudi zake za kuimarisha elimu ya dini katika jamii. Ili kuongeza ufanisi zaidi, Sheikh amewaagiza masheikh wa kata zote kuanza maandalizi ya mapema kwa ajili ya mashindano ya mwakani ili yaweze kushirikisha vijana wengi zaidi na kufanyika kwa ubora wa hali ya juu.

‎Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *