
Manmo mwezi Desemba mwaka uliyopita, Israel ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuitambua Somaliland. Eneo hili lililojitenga lilitangaza uhuru wake kutoka Somalia mnamo 1991 na kutekeleza uhuru wake kikamilifu, lakini Somalia inaendelea kudai eneo hilo, na hakuna nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, hadi wakati huo, iliyoitambua rasmi Somaliland kama taifa huru.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Malengo ya Israel hayakuwa na shaka, lakini yalifichuliwa na chombo cha habari cha Sweden na, siku ya Jumatano ya wiki iliyopita, na shirika la habari la Uingereza Bloomberg, yaliangazia mpango wa Israel wa kujenga kambi ya kjeshi huko Somaliland. Somalia inapinga vikali mradi huu.
“Somalia haitaki eneo lake liingizwe kwenye migogoro ya nje, wala kutumika kwa njia ambayo inaweza kuzidi kuyumbisha eneo ambalo tayari ni dhaifu.” “
Haya ni maneneo ambayo Ali Omar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, aliyasema katika mahojiano na Al Jazeera siku ya Alhamisi, Machi 12, akibainisha kwamba serikali ya Somalia ndiyo pekee mhusika mkuu wa masuala yote ya Somalia.
Lakini si kwa Israel, ambayo iliitambua rasmi Somaliland miezi mitatu iliyopita.
Katika makala ya Bloomberg iliyochapishwa siku iliyopita, Khadar Hussein Abdi, Waziri katika ofisi ya rais wa Somaliland, alikiri kuwepo kwa majadiliano yanayoendelea na Israel kuhusu ushirikiano wa usalama, akidai kwamba suala la kuundwa kwa kambi ya jeshi halijadiliwa, lakini bado hata hivyo halijaondolewa mezani.
Kulingana na chombo cha habari cha Uingereza, mradi huo tayari umeendelea vizuri. Ikinukuu maafisa wa Somaliland wakizungumza kwa sharti la kutotajwa jina na “vyanzo vilivyo karibu na jambo hilo,” Bloomberg inaripoti kwamba Somaliland itaruhusu Israel kukusanya taarifa za kijasusi na kufanya operesheni dhidi ya Wahouthi, kundi lenye silaha la Yemen linalopinga Israel na linaloshirikiana na Iran.
Mwezi Juni mwaka uliyopita, ujumbe wa Israel uliripotiwa kuchunguza ufuo wa Somaliland na kutambua eneo maalum: eneo la milimani takriban kilomita 100 magharibi mwa Berbera, ambapo Falme za Kiarabu, mshirika wa Israel, tayari zina bandari ya kibiashara na uwanja wa ndege wa kijeshi.