
Wafungwa wa magenge hasimu walikabiliana vikali Alhamisi katika gereza moja katika mji wa kaskazini-magharibi mwa Ecuador wa Esmeraldas, na kusababisha vifo vingi, kulingana na polisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Maakabiliano hayo yamezuka katika gereza moja katika mji wa Esmeraldas, kaskazini magharibi mwa Ecuador, karibu na mpaka wa Colombia, ambapo polisi wamesema wamewapata wafungwa 10 wakiwa wamefariki katika vitalu viwili tofauti. Idadi ya waliofariki kutokana na mapigano hayo baadaye ilirekebishwa hadi kufikia angalau 17, mamlaka ya magereza nchini humo imesema.
Picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii na kuthibitishwa na shirika la habari la AFP zinaonyesha wanaume kadhaa wakiwa wamelala chini, bila shati na wakiwa na damu, wakiwemo watu wawili waliokatwa vichwa. Wakati fulani wafungwa wametangaza makabiliano yao ya umwagaji damu moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii, na kuacha miili iliyokatwakatwa, kukatwa kichwa au kuchomwa moto.
Makabiliano haya kati ya magenge hasimu ndani ya magereza yamesababisha vifo vya wtu zaidi ya 500 tangu mwaka 2021. Siku ya Jumatatu, Septemba 22, makabiliano katika gereza jingine, huko Machala (kusini-magharibi), yalisababisha vifo vya wafungwa 13 na mlinzi mmoja.
Vituo vya uendeshaji kwa magenge ya uhalifu uliopangwa
Magereza ya Ecuador yenye msongamano mkubwa mara nyingi ni vituo vya uendeshaji kwa magenge ya uhalifu yaliyopangwa ambayo yamebadilisha Ecuador, ambayo hapo awali ilikuwa kimbilio la amani katika Amerika ya Kusini, kuwa mojawapo ya nchi zenye vurugu.
Uchumi wake wa dola na bandari za Pasifiki huifanya kuwa kituo kikuu cha usafirishaji cha kokeini inayozalishwa katika nchi jirani za Colombia na Peru, wazalishaji wawili wakubwa duniani.
Kulingana na takwimu za serikali, zaidi ya 70% ya kokeini inayozalishwa Amerika Kusini sasa inaondoka kwenye bandari za Ecuador. Idadi kubwa zaidi ya vifo katika vurugu za jela nchini Ecuador ilirekodiwa mnamo mwaka 2021, na vifo vya wafungwa zaidi ya 100 huko Guayaquil (kusini-magharibi).