#HABARI: Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Barke Sehel, amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana ili kufanikisha usawa wa kijinsia.
Akifungua mjadala maalum jijini New York kando ya Mkutano wa 70 wa Hali ya Wanawake Duniani, Jaji Sehel amesisitiza kuwa msaada wa kisheria si nadharia tu, bali ni nguzo muhimu inayotekelezwa kwa vitendo ili kumlinda mwanamke dhidi ya ukatili, ubaguzi, na kutengwa.
Tanzania imeboresha mifumo yake ya kisheria kupitia utungaji wa sheria za msaada wa kisheria ambazo sasa zinajumuisha masuala ya kiraia kama migogoro ya urithi, ardhi, na familia, tofauti na awali ilipojikita kwenye jinai pekee.
Hatua hizi zinaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo imesogeza huduma za haki karibu zaidi na wanawake wa vijijini na makundi yaliyotengwa.
Jaji Sehel ametoa wito kwa mataifa na wadau wa kimataifa kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu ili kuhakikisha hakuna mwanamke anayebaki nyuma katika harakati za kutafuta haki.
Amesema kuwa upatikanaji wa haki ni msingi wa maendeleo jumuishi, kwani uwezo wa mwanamke kushiriki katika siasa na uchumi unategemea sana uwezo wake wa kudai na kutetea haki zake kisheria.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.