#HABARI: Mkoa wa Mbeya umekumbwa na hofu baada ya kurejea kwa mtindo wa kinyama wa uporaji kwa kutumia nondo na nyundo, ambapo watu sita wamepoteza maisha katika matukio tofauti.

Kati ya waliofariki, wanne wanadaiwa kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuhusika na mashambulizi hayo ya usiku yanayolenga vichwa vya wahusika, jambo lililosababisha vifo na vilio katika jamii.

Hali ya usalama mkoani humo imezidi kuwa tete huku majeruhi kadhaa wakiendelea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mafuvu ya kichwa katika hospitali mbalimbali kufuatia vipigo hivyo vizito.

Mamlaka na vyombo vya dola vimeanza uchunguzi wa kina kudhibiti mnyororo huo wa uhalifu uliowahi kutikisa amani ya mkoa huo huko nyuma, huku wananchi wakihimizwa kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kushirikiana na polisi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *