#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Agnesta Kaiza, ameahidi kufikisha bungeni changamoto ya upungufu wa mabweni inayoikabili Shule ya Msingi ya Viziwi Buguruni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza shuleni hapo Mhe. Agnesta amebainisha kuwa ujenzi wa mabweni hayo utawasaidia wazazi kuwa na muda wa kufanya shughuli za kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi shuleni kuwasubiri watoto wao ili kuwarudisha nyumbani.
Mhe. Agnesta ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni sehemu ya kuwapa mkono wa heri kuelekea sikukuu za Iddi na Pasaka.
Msaada huo unalenga kuwafariji na kuwapunguzia mzigo wa mahitaji wanafunzi hao, huku Mbunge huyo akisisitiza kuwa kundi hilo linahitaji uangalizi wa kipekee kutoka serikalini na kwa wadau wa maendeleo.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Richard Kweka, amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada na ahadi yake ya kutafuta suluhu ya kudumu ya miundombinu.
Aidha, Kaka Mkuu wa shule, Salehe Abdala, ameomba jamii kuendelea kujenga upendo na mshikamano huku akisihi mamlaka husika kutatua changamoto mbalimbali zinazokwaza ustawi na masomo ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia shuleni hapo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.