#HABARI: Wizara ya Katiba na Sheria imezindua rasmi huduma ya “Sema na Waziri” Machi 17, 2026, inayolenga kuwasaidia wananchi kuwasilisha changamoto zao za kisheria kwa njia ya simu bila malipo.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Homera, amesema kuwa huduma hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutumia mifumo ya kidijitali kuwafikia wananchi kwa urahisi na kuhakikisha wanasikilizwa na kupata unafuu wa kisheria popote walipo.

Kupitia programu hiyo, Waziri atakuwa akizungumza moja kwa moja na wananchi angalau mara tatu kwa mwezi kupitia namba za simu 0800004004 au 0262160360, pamoja na namba ya WhatsApp 0739101910.

Mhe. Homera amesisitiza kuwa mfumo huu unalenga kuimarisha uwajibikaji na kuboresha utoaji wa haki kwa kurahisisha mawasiliano kati ya viongozi wa juu wa wizara na wananchi wenye kero mbalimbali.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mhe. Zainab Katimba amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo cha huduma, jumla ya malalamiko 2,023 yamepokelewa, huku 1,394 kati yake yakiwa yamefanyiwa kazi.

Malalamiko hayo yanahusisha masuala nyeti kama migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, matunzo ya watoto, na ukatili wa kijinsia, hali inayoonyesha uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *